Kiri Neno

Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, maana maagizo yako yote ni ya haki (ZABURI 119:172)

Neno la Mungu ni hazina ilioje. Limejaa hekima, maelekezo, ukweli, na kila kitu kile tunahitaji ili tuishi maisha ya mafanikio yenye lengo na nguvu. Tunahitaji kujumlisha Neno katika maombi yetu, tukilikiri juu ya kila jambo na hali. Neno kiri linamaanisha “kusema kitu kimoja kama vile,” kwa hivyo tukikiri Neno, tunasema vitu kama vile Mungu anavyosema; tunajiweka katika makubaliano naye. Iwapo kweli tunataka uhusiano wa ndani na wa kusisimua na Mungu, tunahitaji kukubaliana naye na hakuna kitakachotusaidia kufanya hivyo kuliko kukiri Neno la Mungu. Kukiri kwetu huimarisha ufahamu wetu wa Neno na imani yetu katika Mungu, ambayo huzidisha usawa na athari ya maombi yetu.

Ili kukiri Neno, tunahitaji kujua Neno, kwa sababu tunaweza kukubaliana tu Mungu iwapo tunajua alichofanya na kile alichosema. Huwa ninakutana na watu wanaomwambia Mungu awape kitu ambacho tayari wanacho au kuwafanya kuwa vile tayari walivyo, na huwa nataka kuwaambia, “Acheni kuomba hivyo! Tayari Mungu alimaliza kazi mnayomwambia afanye.” Hakuna haja ya kumwomba Mungu akubariki kwa kuwa tayari ashakubariki. Itakuwa bora kusema, “Mungu, asante kwa kuwa kulingana na Neno lako, nimebarikiwa.” Maombi ambayo unamwomba kitu ambacho tayari ametoa hayana maana. Tukiomba Mungu kwa kutumia Neno lake au kumkumbusha, tunaheshimu Neno lake na kujikumbusha vile linavyosema. Kila wakati tunapozungumza Neno lake, nguvu zinaachiliwa kutoka mbinguni kuleta mabadiliko duniani!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Neno la Mungu kutoka katika kinywa chako kwa imani ni mojawapo ya nguvu kuu mbinguni na duniani.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon