Kitendo cha Upendo Hudumu Milele

Kitendo cha Upendo Hudumu Milele

Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 1 WAKORINTHO 13:1

Wingi wa vitu tunavyovipa muda na nguvu zetu ni vitu ambavyo vinapita na wakati, vitu ambavyo havitadumu. Tunang’ang’ana kutengeneza pesa, kujenga biashara, kupata mafanikio makubwa, kuwa maarufu, kumiliki mijengo, magari na mapambo. Tunataka kupanua mawazo yetu na kuona ulimwengu, ilhali hivi vitu vyote ni vya muda tu. Vyote vitafika mwisho.

Ni upendo tu usiofika mwisho. Kitendo cha upendo huendelea na kudumu milele.

Shukuru kuwa Mungu huturuhusu kuwa na athari ya kudumu anapotuambia tuwapende wenzetu. Henry Drummond anasema kwamba “kupenda kwingi ni kuishi kwingi, na kupenda milele ni kuishi milele.” Ili “kupenda kwa wingi” na “kupenda milele,” ninakuhimiza kwanza kupokea upendo wa Mungu…kisha unaweza kutembea kwa upendo na kila mtu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba ninaweza kuishi maisha kwa njia ambayo ninaweza kuwa na athari ya kudumu. Asante kwa nguvu za upendo. Nisaidie kutumia nguvu hizo na kuleta athari ya milele kwa kuwaonyesha walio karibu nami leo upendo. Nisaidie kujua kilicho muhimu kweli kila wakati.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon