
Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama. MITHALI 19:21
Iwapo hujafanya kazi nzuri ya kuendesha maisha yako, kwa nini usimpe Yule aliyekuumba na kujua mengi kukuhusu kuliko vile utawahi kujijua? Ukianza kuwa na shida na gari lako, unawarudishia waliolitengeneza walitengeneze. Kwa Mungu pia kanuni hiyo ina ukweli. Alikuumba na anakupenda sana. Iwapo maisha yako hayakuridhishi, mpelekee ayatengeneze.
Maisha yako hayatabadilika hadi ufanye uamuzi huo muhimu wa kumpa Mungu maisha yako kudhibiti. Na hizi hapa habari njema: Unapomwomba Mungu kutenda mapenzi yake katika maisha yako, Anasema, “Ndiyo.” Atakarabati maeneo yaliyoharibika, kukupa mwelekeo unasafiri salama katika maisha, na kukupa furaha ambayo hujawahi kujua. Mungu akiwa katika udhibiti, unaweza kushukuru kuwa maisha yako yana mwelekeo mpya, kusudi na tumaini kwa mustakabali.
Sala ya Shukrani
Baba, leo ninakuomba udhibiti maisha yangu kikamilifu. Nisaidie kuachilia! Asante kwa kuwa unaweza kuendesha mambo vizuri zaidi kuniliko. Ninaomba kwamba utaniponya, kunibadilisha, na kujenga upya maisha yangu. Ninashukuru kwa vitu vipya vya kusisimua vilivyo ndani yako na ambavyo viko katika mustakabali wangu.