Kuachilia Makosa Yaliyopita

Kuachilia Makosa Yaliyopita

Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. —WARUMI 8:1

Ni jambo la kufariji kujua kwamba huruma na ukarimu wa Mungu ni mpya kila asubuhi. Kwa sababu ya upendo wake mkuu, Mungu ametoa njia, ili ya kale yaliyopita yasiwe na nguvu juu yako. Hauna lazima ya kuishi katika hukumu na lawama kwa sababu ya makosa yako yaliyopita; unaweza kuishi kwa tumaini kuu na mustakabali wenye nuru mbele yako.

Sehemu ya Mungu ni kutusamehe—sehemu yetu ni kupokea kipawa chake cha msamaha, huruma, na mwanzo mpya. Watu wengi hufikiri, Mungu atanisamehe vipi kama nimefanya vitu vingi? Lakini ukweli ni kwamba Mungu anaweza kushinda na kufanya zaidi kuliko tunavyoweza kufikiria kwamba angeweza kutufanyia (Waefeso 3:20).

Tunapomwomba Mungu atusamehe, ni mwaminifu na wa haki kufanya hivyo. Hutusafisha na kutuondolea dhambi zote (1 Yohana 1:9). Tunasemwa kuwa viumbe vipya tunapoingia katika uhusiano na Kristo (2 Wakorintho 5:17). Ya kale hupita na tunakuwa na nafasi ya mwanzo mpya. Tunakuwa udongo mpya wa kiroho kwa ajili ya Mungu kufanya kazi nao. Anapangia kila mmoja wetu kuwa na mwanzo mpya—tunafaa tu kuhiari kuachilia ya kale na kusonga mbele na Mungu.


Usiruhusu makosa yako ya kale kukurudisha nyuma na kutishia mustakabali wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon