Kuanza kwa Imani, Kumaliza kwa Imani

Kuanza kwa Imani, Kumaliza kwa Imani

Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? —WAGALATIA 3:3

Paulo aliwauliza Wagalatia swali ambalo ninafikiri ni muhimu kwetu kujiuliza leo: Baada ya kuanza maisha yetu mapya ndani ya Yesu kwa kumtegemea Roho, inakuwaje sasa tunajaribu kuyaishi katika mwili?

Kama tu tunavyookolewa kwa neema (Neema ya Mungu tusiyostahili) kupitia kwa imani, na sio kwa matendo ya mwili (Waefeso 2:8-9), huwa tunamkaribia Mungu kila siku kupitia kwa imani. Tunaweza kuanza kila siku kwa kusema, “Bwana, leo ninakutegemea tena. Sio kuhusu kile ninachoweza kufanya kwa nguvu zangu; ni kuhusu kile unachoniita nifanye kwa nguvu zako.”

Tulipookolewa, hatukukuwa katika hali yoyote ya kuweza kujisaidia. Ni kiburi tu, au kukosa maarifa yanayofaa, ndiyo yanaweza kufanya tuhisi tofauti leo—bado hatuko katika hali ya kujisaidia. Lakini kwa shukrani, tuko katika hali timilifu ya kumtegemea Mungu ili tuwe kila kitu tunachohitaji. Mradi tu tunamtazama, tukimwamini kwa kazi yake timilifu katika maisha yetu, tunaweza kutulia na kufurahia kweli maisha ambayo Yesu alikufa kutupatia.

Kuishi katika mwili—tukifanya vitu kwa nguvu zetu wenyewe—husababisha dhiki. Lakini kuishi katika Roho—tukitii, kutumainia, na kumtegemea Mungu—huleta furaha isiyosemeka. Utakapohisi kufadhaika wakati ujao, unaweza kutua na kujiuliza unachojaribu kufanya bila kumwegemea Mungu, na bila shaka utapata chanzo cha dhiki yako.


Ni nguvu za Roho Mtakatifu ambazo hukuwezesha kuishi maisha mapya ndani ya Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon