
Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo. 1 WAKORINTHO 13:13 BIBLIA
Mojawapo ya njia za kuondoa nia yako katika shida au hali sumbufu ni kwenda kumsaidia mtu mwingine. Unapowaonyesha wengine upendo, hubarikiwi tu bali hubadilisha ulimwengu uliokuzunguka. Hizo ndizo sababu mbili kuu za kukufanya uanze kuishi kwa upendo.
Tumejaribu uchoyo, kukata tamaa na kujihurumia—na tumeona tunda baya la mambo hayo. Ulimwengu umeona matokeo ya mambo hayo pia. Lakini shukuru kuwa upendo wa kweli ni tofauti!
Hebu tukubaliane kwamba tutaishi maisha vile Mungu anavyotaka—katika kushukuru na upendo. Kuwa baraka kwa wengine (tazama Wagalatia 6:10), jivike upendo (tazama Wakolosai 3:14), na uishi kama Yesu. Yesu aliamka kila siku na kuzunguka huku na huko akitenda mema (tazama Matendo ya Mitume 10:38). Iwapo tutafuata mfano huo, tuna hakika tutabadilisha dunia.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Baba, kwamba kuna njia bora zaidi ya kuishi maisha yangu kuliko kutafakari shida zangu. Leo ninachagua kwenda nje na kufuata mfano wa Yesu kwa kuwatendea wengine mema. Kwa usaidizi wako, nitakuwa wakala wa mabadiliko katika ulimwengu unaonizunguka.