Leo ni Siku Timilifu ya Kubariki Wengine

Leo ni Siku Timilifu ya Kubariki Wengine

Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. WAEBRANIA 13:16 BIBLIA

Bila shaka baraka za Mungu katika maisha yetu ni kitu cha kutufanya tushukuru, lakini lazima tukumbuke kwamba tumebarikiwa ili tubariki wengine.

Acha nipendekeze majaribio leo. Hebu fikiria: Nitaenda ulimwengu leo na ninaenda kuwa baraka kwa wengine. Halafu kabla hujatoka nyumbani amua kwamba unatoka nje kama mjumbe wa Mungu na kwamba lengo lako ni kuwa mpaji, kupenda watu, na kuongeza faida katika maisha yao.

Unaweza kuanza kutabasamia watu unaokutana nao mchana kutwa. Tabasamu ni ishara ya kukubalika na kupendwa— kitu ambacho watu wengi katika ulimwengu huu hutaka sana. Jiachilie kwa Mungu na uamini atakushughulikia huku ukipanda mbegu nzuri kila mahali unapoenda. Amua kumruhusu Mungu kufanya kazi kupitia kwako leo!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru kwa baraka zilizo katika maisha yangu, Baba. Nisaidie kutumia kile ulichonipa kubariki wengine. Leo, ninachagua kueneza upendo wako, furaha yako, na baraka zako kwa watu nitakaokutana nao.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon