Kuchaguliwa na Mungu

Kuchaguliwa na Mungu

Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda… —YOHANA 15:16

Mungu anapotuchagua kwa sababu ya mipango na makusudi yake ya kiungu, hutumia vigezo tofauti na vile ambavyo ulimwengu hutumia. Ulimwengu huchagua watu kutegemea unavyowaona, talanta zao, elimu, au mafanikio yao, lakini Mungu hafanyi hivyo. Kwa kweli, 1 Wakorintho 1:26-29 inatuambia kwamba Mungu huchagua kile ambacho ulimwengu hufikiri ni kipumbavu ili kuaibisha wenye hekima, na kile ambacho ulimwengu huita kidhaifu ili aviaibishe vyenye nguvu.

Nina furaha sana kujua kwamba Mungu hutuchagua makusudi bila kujali udhaifu wetu. Mungu alipopata wazo la Joyce Meyer Ministries, hakutafuta aliyehitimu sana. Alichagua mtu ambaye alimpenda, mtu ambaye angetia bidii, na mtu ambaye alikuwa amefanya uamuzi. Sikuwa na talanta spesheli, isipokuwa niliwasiliana vizuri, lakini hata wakati huo, kidogo sauti yangu haikuwa ya kawaida. Nina hakika ulimwengu ungenikataa kama mtu ambaye hakuhitimu, lakini nashukuru Mungu hakunikataa.

Kilichokuwa cha kweli kuhusu maisha yangu, ni cha kweli kuhusu maisha yako pia. Huenda watu wakatazama nje, lakini Mungu huutazama moyo. Huenda kuna wengine ambao wamehitimu zaidi au wana talanta, lakini chaguo lake halitegemei jinsi mtu anavyoonekana, elimu, mali, au hata talanta. Inategemea mwelekeo wa moyo wako. Iwapo una moyo mzuri unaomwelekea Mungu na nia iliyo tayari, Mungu anaweza kufanya mengi zaidi kupitia kwa maisha yako kuliko vile ulifikiri kwamba inawezekana.


Tukiendelea kuwa waaminifu kwa Mungu, hatimaye tutafika pale Mungu anataka tuwe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon