Kudumu katika neno

Kudumu katika neno

Ninyi mkikaa ndani yangu , na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Yohana 15:7

Wakristo wengi wanajua umuhimu wa kusoma neno la Mungu lakini ni wachache wanaelewa umuhimu wa kudumu katika neno na kuliruhusu neno kudumu ndani yao.

Ikiwa tutalisoma neno kwa ukakamavu na kuliruhusu kukaa ndani yetu, tutaweza kuyapata maandiko kwa urahisi mno. Na Yesu alisema kwamba tutaomba chochote kile tutakacho na tutapewa.

Kudumu katika neno na kuliruhusu neno lidumu ndani yetu hutufanya wafuasi kamili wa Yesu.( Tazama Yohana 8:31). Inatupa nguvu katika maisha yetu ya maombi, nayo nguvu katika maombi hutupa nguvu dhidi ya adui.

Je, unadumu katika neno la Mungu…..na kuliruhusu lidumu ndani yako? Ikiwa jibu lako ni hapana, nakuhimiza uchukue hatua.Acha kusoma na kutafakari neno lipewe nafasi ya kwanza. Anza kuweka neno akilini mwako, na kuliweka moyoni mwako.Kisha utakapokumbwa na hali za maisha, utakuwa umejiandaa kushinda vita hivyo.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, ningependa kuwa mfuasi kamili na kuenenda katika nguvu iliyo katika kudumu kwa neno lako. Niongoze ninaposoma neno kwa ukakamavu na hata kulitia moyoni mwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon