Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. —WAEFESO 1:7
Mojawapo ya vizuizi vikubwa sana vinavyotuzuia kusherehekea maisha ambayo Yesu ametupatia bure ni utambuzi wetu wenyewe wa dhambi. Dhambi ni tatizo kwa kila mtu, lakini haina lazima ya kuwa tatizo tatanishi jinsi tunavyoelekea kuifanya kuwa.
Kwamba tunang’ang’ana na dhambi zetu ni maelezo yasiyofafanuliwa kwa urefu. Tunapofanya kosa, kuonyesha udhaifu, au kushindwa kwa njia yoyote, mara nyingi huwa tunashuku kwamba Mungu anatupenda, kushangaa iwapo ana hasira nasi, na kujaribu kufanya kila aina ya matendo mazuri ili kufidia makosa yetu, na kusalimisha furaha yetu kama dhabihu ya makosa yetu.
Mungu anatamani kutupatia kipawa cha msamaha. Tukikiri dhambi zetu kwake, anatusamehe dhambi zetu, kuziweka mbali naye vile mashariki ilivyo mbali na magharibi, na kuzisahau kabisa (Zaburi 103:12). Lakini ili nasi tufaidi kutokana na msamaha huo, ni muhimu tuupokee kwa imani.
Nilipokuwa aaminiye mpya, kila usiku ningemsihi Mungu kunisamehe kwa dhambi zangu za kale. Jioni moja nilipokuwa nimepiga magoti kando ya kitanda changu, Bwana alizungumza na moyo wangu, “Nilikusamehe mara ya kwanza ulipoomba, lakini hujapokea kipawa changu kwa sababu hujajisamehe.”
Yesu alibeba dhambi zako msalabani, na anatoa msamaha. Huna lazima ya kujishtumu zaidi tena.