Kufuata Mfano wa Mungu

Kufuata Mfano wa Mungu

Mungu akaiona nuru ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. MWANZO 1:4

Kama waaminiyo, mimi na wewe tuna kiwango kimoja cha maisha kama ya Mungu na tunaweza kuyapata maisha haya. Maisha yake hayajajaa hofu, msongamano wa mawazo, wasiwasi, dukuduku au mfadhaiko. Na tunashukuru kwamba, si lazima maisha yetu yawe hivyo. Badala ya kuwa na wasiwasi, Mungu huchukua muda kufurahia viumbe wake, kazi ya mikono yake.

Katika kisa cha Uumbaji kama kilivyorekodiwa katika Mwanzo 1, mara nyingi Andiko husema kwamba baada ya Mungu kuumba sehemu fulani ya ulimwengu ambao tunaishi, aliona kuwa ilikuwa njema (njema, yenye kupendeza, inayofaa na yenye kuvutia) Akaiidhinisha. (tazama mistari 4, 10, 12, 18, 21, 25, 31.) Inaonekana kwangu kwamba ikiwa Mungu alichukua muda kufurahia viumbe wake, kazi yake, basi mimi na wewe tunaweza kufurahia kazi yetu. Tunaweza kufurahia kwa shukrani tukijua kuwa Mungu anatupatia uhuru wa kufurahia mafanikio yetu.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa mfano ulionionyesha na kwa maisha ambayo umefanya niweze kuishi. Si lazima niishi maisha ya kusongwa na mawazo, hofu, au wasiwasi. Nisaidie kusahau vitu hivyo na kufurahia maisha ambayo umenipa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon