Kufurahia katika Maendeleo

Kufurahia katika Maendeleo

Maana wewe umekuwa msaada wangu, na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. ZABURI 63:7

Tunaweza kushukuru kuwa Mungu anataka tufurahie. Kwa kweli, Biblia inajadili kufurahia angalau mara 170. Na tukisoma Neno, tunapata kwamba, kufurahia ni kitendo cha kuonyesha hisia.

Huenda tukapiga makofi watoto wetu wakionyesha kupiga hatua, huenda tukapiga nduru tukifanikiwa, au huenda tukacheka tukifikiria au kuongea kuhusu wema wa Mungu. Tunaweza pia kufurahia tukipiga hatua katika ukuaji wetu wa kiroho.

Biblia inasema kwamba njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu (tazama Mithali 4:18). Iwapo unaweza kutazama nyuma na kusema, “Nimebadilika. Tabia zangu zimebadilika kidogo. Nina subira kidogo. Mimi ni mkarimu zaidi. Mimi si mchoyo sana, basi unaweza kusherehekea. Kila mabadiliko yanastahili wakati mchache wa kusherehekea!


Sala ya Shukrani

Baba, ninapoona mabadiliko kidogo katika maisha yangu, nisaidie kukumbuka kutenga muda mchache wa kufurahia. Asante kwa kunipa roho wa furaha badala ya roho nzito. Nitasherehekea na kufurahia ndani yako leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon