Kuhesabu tena Ushindi

Kuhesabu tena Ushindi

Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe! —1 SAMWELI 17:37

Wakati ambao Daudi alijitolea kwenda kupigana na Goliathi, hakuna hata aliyemhimiza. Kila mtu akiwemo mfalme alimwambia alikuwa mdogo sana, hakuwa na tajriba, alikuwa mdogo, na hakuwa na silaha zilizofaa. Lakini Daudi alijitia moyo kwa kuhesabu tena ushindi ambao Mungu alikuwa amempa katika siku zilizopita. Mwishowe, Sauli akamwambia aende, lakini bado hakuamini kwamba Daudi angeweza kushinda.

Utakuwa na nyakati nyingi sana katika maisha ambazo utaachwa bila mtu wa kukuhimiza, na katika nyakati hizo, utahitaji kumtegemea Mungu peke yake. Adui huwa haachi kujaribu kutukatisha tamaa. Anataka kutuzuia kuwa waaminifu kwa kile Mungu anataka tufanye. Leo, ninataka kuwahimiza kwamba, ukiwa na Mungu unaweza kufanya chochote unachohitaji kufanya.

Wakati ule ambao unalazimika kungoja kitu kwa muda mrefu , au inapoonekana kwamba kila kitu na kila mtu ameinuka kinyume nawe, badala ya kuwa na mawazo mabaya na kushushwa moyo, mwambie Mungu, “Bwana, nitakuwa mwaminifu kwako. Ninakumbuka ulichofanya maishani mwangu katika siku zilizopita. Ninajua utanikomboa tena. Ninakutumainia kunipitisha hapa.” Mungu yuko karibu nawe kuliko vile unavyoweza kutambua, na hatakuangusha.


Mungu ni nguvu yako, na kila kitu kinawezekana kwake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon