Kuingia Rahani kwa Bwana

Kuingia Rahani kwa Bwana

Heri walio kamili njia zao, waendao katika sheria ya Bwana. —ZABURI 119:1

Kuna uhuru wa kiungu na utulivu ambao huja unapopenda Neno la Mungu kwa kweli—unapolisikia, lipokee na ulitii. Hata katika hali ngumu, maisha yako yatakuwa huru kutokana na dhiki pamoja na masikitiko. Furaha yako ni kamilifu unapomkaribia Mungu kupitia kwa Neno lake, ukiamini ahadi zake juu ya maisha yako na kutii sheria zake.

Ufunguo wa kushinda matatizo unayokabiliana nayo maishani ni kuamini Neno la Mungu na kutii kile ambacho Mungu anaweka katika moyo wako ufanye. Kusimama kwa Neno lake hukukomboa kutokana na kung’ang’ana ndipo upate kupumzika katika ahadi za Bwana. Waebrania 4:3 inasema: “Kwa kuwa sisi ambao tumeamini (tumeshikilia na kuamini na kumtegemea Mungu) huingia katika raha hiyo.”

Ukihisi kushindwa leo—iwapo umezidiwa na shida—jambo zuri unaloweza kufanya ni kuchukua muda kusikiliza, kupokea, na kutii Neno la Mungu. Hapo ndipo utakapopata maneno ya uzima. Mara tu utakapoanza kuamini Neno la Mungu, furaha yako itarudi na utapata utulivu tena.


Maisha ya utulivu ndani yake ndipo mahali Mungu anataka uwe kila siku ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon