Kuishi katika Sasa

Kuishi katika Sasa

Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. —1 YOHANA 3:2

Uteuzi tunaofanya leo utaamua iwapo tutafurahia sasa au tutaiharibu kwa kuwa na wasiwasi. Wakati mwingine tunaishia kukosa muda wa leo kwa sababu tuna wasiwasi sana kuhusu kesho. Tutakuwa na hekima tukidhamiria kulenga kile Mungu anataka tufanye sasa.

Ni muhimu kuelewa kwamba Mungu anataka tujifunze jinsi ya kuwa watu wa sasa. Kwa mfano, 2 Wakorintho 6:2 inasema, “Tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa” na Waebrania 4:7 inasema, “Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.”

Tungekuwa wenye kuzalisha matunda zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu, na kuwa na furaha zaidi katika maisha yetu iwapo tutaamua kuishi sasa. Mara nyingi huwa tunatumia muda wetu wa kiakili katika ya kale au yajayo. Tunapokosa kujitoa kwa kile tunachofanya sasa, tunakuwa wepesi wa kufadhaika na kuwa na wasiwasi. Lakini tukiishi katika sasa, tutampata Bwana huko na sisi. Haijalishi hali ambazo maisha yatatuletea, tutajua kwamba leo—sasa hivi—ni sehemu ya mpango wa Mungu, na atatupitisha hapo iwapo tutamwamini.


Wakati ambao uko nao sasa ni wa thamani. Usiharibu “sasa” yako na wasiwasi kuhusu kesho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon