Kuishi kwa Kukiuka Hisia Zako

Kuishi kwa Kukiuka Hisia Zako

Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. 2 WAKORINTHO 12:10

Kuna siku ambayo huenda tukahisi vizuri au vibaya, furaha au huzuni, kusisimka au kukata tamaa, na maelfu ya vitu vingine. Ingawa hisia zinaweza kuwa na nguvu sana na kuwa mzigo, si lazima tuziachilie kutawala maisha yetu.

Tunaweza kujifunza kudhibiti hisia zetu badala ya kuziruhusu kutudhibiti. Huu umekuwa mojawapo ya ukweli muhimu wa kibiblia ambao nimejifunza katika safari yangu na Mungu. Umekuwa pia ukweli ambao unaniruhusu kufurahia maisha daima.

Iwapo ni lazima tungoje kuona vile tunavyohisi kabla tujue iwapo tutafurahia siku, basi tunazipa hisia udhibiti juu yetu. Lakini shukuru kwamba tuna nia huru na tunaweza kufanya uamuzi ambao hautokani na hisia. Iwapo tuna hiari kufanya uamuzi ulio sahihi bila kujali tunavyohisi, Mungu atakuwa mwaminifu kila wakati kutupatia nguvu za kufanya hivyo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kuwa silazimiki kuacha hisia zangu zinidhibiti. Ninashukuru sana kwamba si lazima ningoje kuona vile ninavyohisi kila siku kabla nijue vile nitakavyotenda. Kwa usaidizi wako, nitaishi kwa kukiuka hisia zangu—nitaishi maisha yaliyojaa furaha ambayo Yesu alikuja kunipa!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon