Kuishi kwa Kushangaa

Kuishi kwa Kushangaa

Wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. LUKA 4:32

Ninafikiri kwamba mara nyingi tunaachilia kile ambacho kinafaa kuwa kitu maalum kwetu—vitu ambavyo tunafaa kushukuru sana kwa ajili yavyo—tunavichukulia kama vitu vya kawaida. Miaka mingi iliyopita, nilikuwa “nikimnong’onezea” Bwana maombi (nikiomba lakini kama kumnong’onezea wakati huohuo) na nikasema, “Bwana, kwa nini hivyo vitu maalum vinavyosisimua visifanyike katika maisha yangu kama vilivyokuwa vikifanyika nilipokujua mara ya kwanza?”

Na sitasahau kile Mungu aliuambia moyo wangu kwa uwazi. Alisema, “Joyce, bado unafanya vitu vilevile kila wakati, ni vile tu ulivizoea.”

Ninaamini kwamba iwapo tutaendelea kushangazwa na vitu ambavyo Mungu anafanya katika maisha yetu—hata vitu vidogo—hatutakosa kuwa na tumaini. Ninakuhimiza kutambua ulicho nacho, kuwa mwenye shukrani, na uamue kuishi kwa kushangaa…mdomo wazi, kukodoa macho na kusema, “Lo! huyo alikuwa Mungu!”


Sala ya Shukrani

Ninashukuru kwamba unafanya vitu maalum katika maisha yangu kila mara, Bwana, na ninaomba kuwa nitavitambua na kuwa mkarimu katika sifa zangu na shukrani. Nisaidie kuishi nikishangaa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon