Kuishi Maisha ya Kiasi

Kuishi Maisha ya Kiasi

Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Wafilipi 4:5 Biblia

Kudumisha maisha ya kiasi bila shaka ni mojawapo ya changamoto kubwa sana ambazo tunazo. Ninakuhimiza kuchunguza maisha yako kila mara na ujiulize kwa uaminifu iwapo umeruhusu eneo lolote kutoka nje ya kiasi. Huenda ukosefu wa kiasi ndio sababu ya kukosa kufurahia maisha na pia matatizo mengine mengi.

Kwa mfano: Kazi ni nzuri na tunashukuru kwa nafasi ya kufanya kazi lakini ikiwa nyingi sana husababisha mfadhaiko. Chakula ni kizuri, na bila shaka tunashukuru kwa kuwa tuna chakula cha kula, lakini vile wengi wetu tujuavyo, kingi sana si kizuri. Inawezekana kutumia pesa nyingi sana, lakini inawezakana pia kutotumia pesa nyingi sana. Eneo lolote ambalo liko nje ya kiasi husababisha kuchanganyikiwa na mfadhaiko katika maisha yetu na kuiba furaha yetu.

Sawazisha kila eneo la maisha yako na shughuli zako zote. Fanya vitu vyote kwa kiasi. Hivyo, utaepuka uchovu na kuweza kufurahia kila kitu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa baraka za upaji katika maisha yangu: kazi, chakula na fedha. Nisaidie kuvitazama vitu ifaavyo na kuishi kwa kiasi. Asante kuwa kwa usaidizi wako, ninaweza kuishi na kiasi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon