Kuishi na Kusudi

Kuishi na Kusudi

Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani mwote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. Maana Bwana wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? —ISAYA 14:26–27

Mungu ni Mungu wa kusudio—Husonga kimpango, na hutekeleza mpango wake mtimilifu. Kama wanawe, Mungu hutamani tuwe watu wa kusudi. Kadri tulivyo karibu naye, ndivyo tutakavyoishi na kusudio.

Yesu alijua kusudio lake. Alisema kwamba alikuja ulimwenguni ili tukawe na uzima na kwamba akapate kuharibu kazi za shetani (Yohana 10:10, 1 Yohana 3:8).

Kulingana na kusudi letu maalum, hili hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kutoka msimu mmoja wa maisha hadi mwingine, lakini Mungu ana kusudi jumla ambalo sisi wote tunaweza kuchagua kuishi ndani yake kila siku.

Kwa mfano, tunawapenda wengine, sio kwa sababu huwa tunahisi kuwapenda, lakini kwa sababu tunakusudia kuwapenda wengine. Jambo lilo hilo ni kweli tunapotoa, kuonyesha rehema, kudhihirisha huruma, kusamehe na vitu vingine vingi. Upendo, furaha, amani, huruma, uvumilivu na wema na matunda mengine yote ya Roho ni yetu kufurahia na kuachilia kwa wengine tukikusudia kufanya hivyo. Tunafanya mambo haya, sio kwa sababu tunahisi kuna haja ya kufanya hivyo, lakini kwa sababu ni mambo tuliyoitiwa kufanya.


Furaha na amani havifanyiki kwa ajali; huja ukichagua kuishi maisha yako na kusudi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon