Kujenga Imani Kuu

Kujenga Imani Kuu

Yesu akajibu, akamwambia, mwaminini Mungu. MARKO 11:22

Imani ndogo inaweza kuwa imani kubwa tunapoitumia. Tunapochukua hatua kumwamini Mungu, tunazoea uaminifu wake na hilo linatuhimiza kuwa na imani kubwa zaidi. Imani yetu inapojengeka na kukua, shida zetu zinakuwa na nguvu chache zaidi juu yetu na tunakuwa wenye wasiwasi kidogo— hicho ni kitu cha kushukuru kwacho.

Tunaweza kuchagua kufikiria kuhusu kile ambacho Mungu anaweza kufanya badala ya kile tusichoweza kufanya. Tukifikiri kuhusu ugumu wa hali yetu kila mara, huenda tukakata tamaa, na hiyo ina maana kwamba tutahisi kwamba hatuwezi kupata vile tutakavyoondoka kwenye hali hiyo. Tutahisi kwamba tumefungika, halafu ni rahisi kushikwa na hofu na kuanza kufanya vitu bila kufikiria hivyo kufanya hali hiyo iwe hata ngumu zaidi. Lakini Biblia inatuambia kwamba wakati wote Mungu hufanya njia (tazama 1 Wakorintho 10:13). Hata ingawa huenda usione njia ya kuondokea sasa hivi, moja ipo tayari na Mungu atakufunulia unapomwamini.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba imani yangu inaweza kukua na kuwa yenye nguvu ninapotia imani yangu ndani yako. Wewe ni mkubwa kuliko shida yoyote ambayo itawahi kunikabili. Ninapokutazama, ninajua kwamba wasiwasi na mtamauko utafifia. Asante kwa uaminifu wako na kazi yako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon