Kujitoa Wakfu kwa Matumizi Yake

Kujitoa Wakfu kwa Matumizi Yake

Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihi iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. —WARUMI 12:1

Ili Mungu atutumie, lazima tuyatoe wakfu maisha yetu kwake. Tukitoa wakfu maisha yetu kwa Mungu kwa kweli, tunajitua mzigo wa kujaribu kutawala maisha yetu.

Lazima kuyatoa maisha yako wakfu kwa Mungu kuwe na ukweli. Ni rahisi kuimba na watu wengine wimbo kama “Ninasalimisha yote.” Tunaweza hata kuwa na mihemko ya kihisia, lakini mtihani wa kweli unapatikana katika maisha ya kila siku wakati ambao hali haziendi vile tulivyofikiria zitaenda. Kutoa wakfu roho, nafsi na mwili wako kwa Mungu ni zaidi ya wimbo—ni uamuzi wa kila siku.

Sehemu muhimu ya kumkaribia Mungu ni kuwa na moyo uliojitoa wakfu. Tunapochagua kuishi kwa kutii Neno la Bwana, humpendeza Mungu pakubwa. Ukijitoa wakfu kwake kwa uaminifu, unaingia kwenye uhusiano mpya wa kiwango cha kina kirefu ambao huongeza nguvu zako na kuongeza msisimko kwa kila siku ya maisha yako.


Itoe wakfu kila sehemu ya maisha yako kwa Mungu na uache Roho Mtakatifu akufanye chombo kinachofaa kwa matumizi ya Bwana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon