Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? WARUMI 8:31
Kisa kinaelezwa kuhusu mvulana mdogo aliyesikika akijisemesha nyuma ya nyumba. Alikuwa amevaa kofia ya besiboli na alikuwa amebeba mpira na gongo: “Mimi ndiye mshambuliaji mkubwa sana duniani,” akatangaza. Kisha akarusha mpira hewani, akaurusha, akaurukia lakini ukakosa kulenga. “Lenga moja!” akapiga kelele. Akauokota mpira na kusema tena, “Mimi ndiye mshambulizi mkubwa sana duniani!” akaurusha mpira hewani. Akaruka tena na kuukosa. “Shambulio la pili!” akapiga kelele. Akanyosha kofia yake na kusema mara ya mwisho, “Mimi ndiye mshambulizi mkubwa sana duniani!” Akarusha mpira juu hewani na kuurukia. Akaukosa. “Shambulio la tatu! Waah!” akatamka kwa mshangao. “Mimi ndiye mtupaji mkubwa sana duniani!”
Nia yenye shukrani, chanya na isiyokubali kukata tamaa itabadilisha vile unavyoonekana na kubadilisha maisha yako pia.
Sala ya Shukrani
Baba, nisaidie kuona maisha kwa njia mpya. Ninakushukuru kwamba kwa sababu uko nami, sihitaji kuhisi kushindwa tena. Una mpango juu ya maisha yangu. Nikiruka na kukosa, inamaanisha tu una kitu kilicho bora zaidi kwa ajili yangu.