kukua katika ufahamu

kukua katika ufahamu

Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; Isaya 11:2-3

Yesu aliishi maisha yake kwa ufahamu. Utambuzi wake haukutegemea hisia za kimwili – ilikuwa matokeo ya ushirika wake wa karibu na uhusiano na Baba yake Mungu.

Zawadi hiyo hiyo ya ufahamu inapatikana kwako na mimi kupitia uhusiano wetu na Mungu. Hivyo inafanyaje kazi? Kabla ya kufanya chochote, lazima uangalie haraka na roho yako ili uone kama jambo ambalo unakaribia kufanya ni sawa. Ikiwa una amani, basi endelea. Lakini kama una wasiwasi, kuchanganyikiwa au kutokuwa na hakika, tulia kwanza.

Kwa mfano, wakati mwingine nimekuwa katika maduka ya kununua tayari kununua kitu, lakini kabla ya kufikia hapo, nilihisi kuchanganyikiwa katika roho yangu, ambayo ilikuwa kama sauti kutoka kwa Roho Mtakatifu nisinunue.

Kitu cha kusisimua juu ya wakati kama huo ni kila wakati wewe na mimi huchagua kusikiliza na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, roho zetu zinakua na nguvu katika Mungu, na nguvu zaidi na zaidi ya Mungu hutolewa katika maisha yetu kufanya kazi katika matunda ya Roho.

Jipeane kwa Roho Mtakatifu na ufuatie miongozo yake na utakua katika ufahamu huo ule ambao Yesu alitembea.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, sitaki kufanya maamuzi kulingana na tamaa zangu za juu au za ubinafsi. Ninataka kutembea katika ufahamu. Ninapokuangalia wakati ninafanya maamuzi, haribu tamaa nilizo nazo zisizo zako, na unipe amani kufuata njia yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon