Kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. 1 PETRO 5:5
Unyenyekevu ni kujua hatuwezi kufanikiwa kwa kujiamini na kwa jitihada zetu za kibinadamu. Badala yake, tunamwamini Mungu, tukishukuru kwamba anafanya tusichoweza kufanya. Tunapofuata uongozi wa Roho Mtakatifu na kumwegemea nyakati zote, wakati wote hutupa vifaa vya kufanyia kile tunachofaa kuwa tukifanya. Kushindwa kwingi kwa binadamu hutokana na kujaribu kufanya vitu katika nguvu zao bila kumtegemea Mungu.
Nimegundua kwamba ninapohisi kufadhaika, ni kwa sababu ninasukumiza jitihada za kimwili kwa kujaribu kufanya kitu ambacho Mungu peke yake anaweza kufanya. Ninapendekeza kwamba unapohisi kufadhaika, simama na ujiulize iwapo unafanya kitu kile kile. Matendo ya mwili ni sawa na mtamauko, na matendo ya mwili yana maana kwamba ninafanya kazi bila Mungu.
Tunaweza kuishi maisha ya ushindi yaliyojaa furaha tukitambua kwamba Mungu huwasaidia wale wanaojua hawawezi kujisaidia—wale wanaotambua wanamtegemea Mungu kabisa na wanashukuru kwamba atawapa kila kitu wanachohitaji.
Sala ya Shukrani
Baba ninashukuru kwamba sihitajiki kutegemea nguvu zangu binafsi au jitihada nzuri kabisa ili kufanikiwa maishani. Asante kwamba uko hapa kunielekeza na kunisaidia kila siku. Ninakuamini na ninayaweka maisha yangu mikononi mwako.