Kuomba, Kusema na Kufanya

Kuomba, Kusema na Kufanya

Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. WARUMI 12:3 BIBLIA

Imani inapewa kila mtu, kulingana na Warumi 12:3, lakini lazima hiyo imani iachiliwe iwapo itafanya kitu kinachoonekana. Huenda ikafikiriwa kwamba ni kuwa kiroho kusema, “Nimejaa imani,” lakini, je, unaitumia imani yako? Imani huachiliwa kwa kuomba, kusema na kufanya chochote Mungu anachotuambia tufanye:

• Kuomba: Tunamwalika Mungu kuhusika katika hali zetu kupitia kwa maombi yetu.

• Kusema: Ni muhimu kwamba tuongee kama tunaoamini kuwa Mungu anafanya kazi kwa ajili yetu

• Kufanya: Kiambato cha tatu katika kuachilia imani yako ni kufanya chochote unachoamini Mungu anakwambia ufanye.

Shukuru kwa imani ambayo Mungu amekupa na uanze kuifanyisha kazi katika maisha yako kwa kuomba, kusema na kufanya.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kuwa ninaweza kuachilia imani yangu tu kwa kuja kwako kwa maombi, huku nikitamka ahadi zako na kufanya unachoniambia nifanye. Nisaidie kusimama katika imani wakati ambao hali zinanipinga. Ninakushukuru kwa kuwa ninaweza kukuamini kabisa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon