Kuomba Maombi ya Imani na Ujasiri

Kuomba Maombi ya Imani na Ujasiri

Basi kwa kuwa mna taraji la namna hii, twatumia ujasiri mwingi. 2 WAKORINTHO 3:12

Mungu anatafuta wanaume na wanawake ambao wataomba maombi ya ujasiri. Mojawapo ya maombi ambayo huwa nasikia watu wakiomba kila mara ni yale naita maombi ya “tu.” Ombi la thibitisho husikika hivi” “Sasa Bwana, tunakuomba tu utulinde,” au “Ee Mungu, iwapo tu utatusaidia katika hali hii.” Haya maombi hutufanya tusikike kama ambao tunaogopa kumwomba Mungu vitu vingi.

Likitumiwa hivi, neno “tu” linamaanisha kitu kidogo kisichotosha au kisichopita mipaka. Mungu anataka kutupatia zaidi, mengi ya ajabu kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo (tazama Waefeso 3:20)—hicho ni kitu cha kushukuria! Mungu anataka kusikia maombi ya ujasiri na tumaini ambayo yamejaa imani yakiombwa na watu wenye shukrani walio salama katika uhusiano wao naye. Usiwe mwoga kumwomba Mungu vitu vingi kwa sababu anakupenda na anataka kukufanyia mengi zaidi kuliko vile unavyoweza kuwaza.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unaniruhusu kuomba maombi ya ujasiri na imani. Ninajua wewe si Mungu wa inayotosha tu— Wewe ni Mungu wa zaidi ya kutosha. Ninakuondolea mipaka leo, na kukuamini kufanya kitu kikubwa katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon