Kuongozwa na Roho

Kuongozwa na Roho

Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. — WAGALATIA 5:16

Ni jambo la kupendeza kwamba katika Wagalatia 5:16, Paulo hakusema hamu, au tamaa za mwili, hazitawashika wana wa Mungu. Alisema kwamba tunaweza kuchagua kuongozwa na Roho Mtakatifu, na kwa kufanya uteuzi huo, hatutakubali majaribu yatakayojaribu kututenga na Mungu.

Kuna vitu vingi vinavyojaribu kutuongoza—watu wengine, shetani, miili yetu wenyewe (mwili wetu, nia, hiari au hisia). Kuna sauti nyingi ulimwenguni zinazotungumzia, na mara nyingi huwa kadhaa kwa wakati mmoja.

Ili kuishi katika uhusiano wa karibu Mungu, ni muhimu kwamba tuchague kuongozwa na Roho Mtakatifu badala ya hizo sauti zingine. Ni yeye peke yake anayejua mapenzi ya Mungu na ametumwa kuishi ndani ya kila mmoja wetu, kutusaidia kuwa kila kitu ambacho Mungu ametuumba kuwa, na vyote ambavyo Mungu anataka tuwe navyo.

Kuongozwa na Roho ina maana kwamba anatuongoza kwa amani na kwa hekima, vilevile kwa Neno la Mungu. Huzungumza kwa sauti tulivu, ndogo katika mioyo yetu tunapotafuta kumwishia Mungu maisha yetu. Kadri tunavyofuata uongozi wake, ndivyo tutakavyokuwa washindi katika maisha.


Ninakuhimiza kuanza kila siku kwa kusema, “Roho Mtakatifu, nitasikiliza uongozi wako leo. Nipe hekima na amani ili niweze kusonga katika kila hatua kulingana na uongozi wako.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon