Kuonyesha Rehema

Kuonyesha Rehema

Heri wenye rehema maana hao watapata rehema! —MATHAYO 5:7

Kuwa mwenye rehema inaweza kufafanuliwa kama kutoa wema usiostahiliwa. Mtu yeyote anaweza kuwapa watu wanachostahili. Huchukua mtu anayetamani kuwa karibu na Mungu kuwaonyesha watu wema wakati ambao hawaustahili.

Kisasi husema, “Ulinitesa, kwa hivyo nitakutesa.” Rehema husema, “Ulinitesa lakini nitakusamehe, nikurejeshe, na kukutendea kama ambaye hujawahi kunidhuru.” Ni baraka ilioje kuweza kuonyesha na kupokea rehema.

Rehema ni sifa ya tabia ya Mungu ambayo huonekana kwa namna anavyokabiliana na watu wake. Rehema ni nzuri kwetu tunapostahili adhabu. Rehema hutukubali na kutubariki wakati ambao tunastahili kukataliwa kabisa. Rehema huelewa udhaifu wetu na upungufu wetu na haituhukumu wala kututoa makosa.

Je, unamhitaji Mungu au mtu kukuonyesha rehema? Bila shaka, sisi wote tunahiitaji kila mara. Njia nzuri ya kabisa ya kupata rehema ni kuwa tukiitoa. Ukitoa hukumu, utapokea hukumu. Ukitoa rehema, utapokea rehema. Kumbuka, Neno la Mungu linatufundisha kwamba tunavuna tunachopanda. Kuwa mwenye rehema! Barikiwa!


Pokea rehema na upendo wa Mungu. Huwezi kutoa kitu usichokuwa nacho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon