Kupambana na Uchungu wa Kihisia

Kupambana na Uchungu wa Kihisia

Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu. 1 PETRO 5:10

Tunapoteseka kihisia, kihisia, huenda tukahisi hasira, dhiki, au hata kukata tamaa, lakini hatuhitajia kuacha mojawapo ya hizo hisia kutudhibiti. Tunaweza kudhibiti hisia zetu kwa usaidizi wa Mungu, na tunaweza kushukuru kuwa hatudhibitiwi na hisia na mihemko yetu.

Watu wengi hutendewa yasiyo haki; hawastahili uchungu wanaopata. Lakini tunaweza kufurahi kuwa, hata kama tunapitia vitu vibaya vya uchungu, tunaye Yesu maishani mwetu kutusaidia na kututia nguvu. Huenda hukuwa na mwanzo mzuri maishani, lakini bado unaweza kuwa na mwisho mzuri. Sahau ya kale na uchukue hatua hadi kwenye maisha mazuri ambayo Mungu alimtuma Mwanawe, Yesu, kununua kwa ajili yako.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kunisaidia kushinda utendewaji wowote usiokuwa wa haki ambao huenda nimepata maishani au nitawahi kuupata. Ninaamini kuwa wewe ni mtetezi wangu na kila mara wewe hufanya yaliyo mabaya kuwa mazuri.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon