Kupenda Maisha Yako

Kupenda Maisha Yako

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. YOHANA MTAKATIFU 10:10

Je, unaamini kuwa Mungu anataka ufurahie maisha yako? Sawa, ndiyo! Kwa kweli, sehemu mojawapo ya hiari ya Mungu ni kwako wewe kufurahia kila wakati wa maisha yako. Ninajua kuwa huu ni ukweli kwa sababu Neno lake linasema hivyo mahali kwingi.

Mfalme Suleiman, ambaye anachukuliwa kuwa alikuwa na hekima, aliandika katika Mhubiri 2:24: “Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.”

Suleiman alisema hayo ili ufurahie matunda ya kazi yako. Tunafaa kujifunza kuthamini raha kwa sababu ni muhimu kwa afya na hali ya kiasi ya mtu. Hii haina maana kwamba maisha yote yatakuwa karamu kubwa au likizo, lakini ina maana kwamba kupitia kwa nguvu za Mungu tunaweza kujifunza kuwa wenye shukrani kwa sababu ya uhai na kufurahia maisha yote.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba Yesu alikuja ili niwe na uzima tele tele. Wakati ambao nyakati ni ngumu na furaha yangu imerudi chini, nisaidie kukumbuka kwamba umeahidi ninaweza kufurahia maisha yangu. Asante kwa furaha, amani na usalama ninaopata ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon