Kupendwa kwa Upendo Mkuu

Kupendwa kwa Upendo Mkuu

Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. — 1 YOHANA 4:10

Wengi wetu wanaamini kwamba Mungu anapenda ulimwengu, lakini hatuna uhakika kabisa kuhusu upendo wake juu yetu binafsi, au huenda tukahisi kwamba Mungu hutupenda tukiwa wazuri, lakini sio tukifanya makosa na kutenda dhambi. Upendo wa Mungu una misingi yake katika jinsi alivyo, sio kwa mambo tunayofanya. Hajawahi kuacha kutupenda, hata kwa sekunde moja ya maisha yetu!

Mungu anakupenda! Wewe ni mtu wa kipekee kwake. Hakupendi eti kwa sababu wewe ni mtu mzuri au unafanya kila kitu inavyofaa. Anakupenda kwa sababu yeye ni upendo. Upendo sio kitu ambacho Mungu hufanya; Yeye ndiye Upendo. Upendo wa Mungu hauwezi kuwa malipo ya matendo mazuri yaliyofanywa wala kustahiliwa kupewa baada ya kufanya jambo fulani. Lazima upokelewe kwa imani. Yeye ni Mungu anayeishi milele, na huwa hachoki. Wengi wetu hufikiri tumemchosha Mungu kwa makosa na kushindwa kwetu lakini huwezi kufanya hivyo. Huenda kila mara asipendezwe na kila kitu unachofanya, lakini anakupenda. Upendo ni tabia yake isiyoshindwa.

Hata utafute vipi vitu vinavyomhusu Mungu, iwapo hujapokea ukweli kwamba Mungu anakupenda, hutafika mbali.

Acha Mungu akupende. Pokea upendo wake kwako. Utafakari. Acha ukutie nguvu na kukuleta karibu na Mungu. Halafu utafute nafasi ya kuwaonyesha wengine upendo huo.


Ungekuwa peke yako duniani, Yesu angepitia mateso yake yote kwa sababu ya wewe peke yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon