Zaidi ya, Tele, Juu ya, na Kupita Kiasi

Zaidi ya, Tele, Juu ya, na Kupita Kiasi

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. —WAEFESO 3:20

Je, umewahi kuwa ukiomba kuhusu watu ambao wanadhurika na kuwa na matamanio makubwa ya kuwasaidia wote? Ninajua bila shaka kwamba nimewahi. Katika nyakati kama hizi ninahisi kwamba matamanio yangu ni makubwa kuliko uwezo wangu, na ni kweli— lakini si makubwa kuliko uwezo wa Mungu.

Wakati kile kitu kinachotukabili katika maisha yetu kinaonekana kuwa kikubwa machoni mwetu hadi macho yetu “yanazunguka kwa kasi,” tunaweza kukumbuka kuwaza kwa mawazo ya Yesu. Katika hali ya kawaida, vitu vingi vinaonekana haviwezekani. Lakini Mungu anataka tuamini kuwa mambo makubwa yatafanyika, tufanye mipango mikubwa, na tumtarajie kufanya vitu vinavyoshangaza kiasi kwamba vitatuacha midomo wazi tukisifu.

Mara nyingi Mungu huwa hawaiti watu wanaoweza; angekuwa akifanya hivyo, asingepata utukufu. Mara nyingi huwa anachagua wale ambao katika hali ya kawaida, hujihisi kwamba hawana uwezo kabisa lakini ndani yao wako tayari kusimama na kuchukua hatua za ujasiri kwa imani. Wamejifunza siri ya kukaa karibu na Mungu na kutumaini kwamba “nguvu zake zinazopita kiasi” zitafanya kazi ndani yao.


Wakati ambao matamanio yako yanaonekana kuwa makubwa kupita kiasi, na huoni vile utakavyoyatimiza, kumbuka kwamba, hata kama hujui njia, unajua Mfanya Njia!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon