Kupitia Motoni

Maana Mungu wetu ni moto ulao (Waebrania 12:29)

Mungu hutamani kula kila kitu ambacho hakimletei utukufu katika maisha yetu. Humtuma Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu sisi waaminiyo, kuwa katika ushirika wa karibu nasi, na kuleta uthibitisho wa kila wazo letu baya, neno, au kitendo. Lazima sisi wote tupitie kwa moto “usafishao” (Malaki 3:2).

Inamaanisha nini kupitia katika moto ulao? Ina maana Mungu atatushughulikia. Atashughulika kubadilisha nia zetu, matamanio, njia, fikra na mazungumzo. Atatuzungumzia kuhusu vitu vilivyomo mioyoni mwetu ambavyo havimpendezi, na atatuambia tubadilishe hivyo vitu kwa usaidizi wake. Wale ambao wanapitia katika moto badala ya kuutoroka ndio watakaomletea Mungu utukufu mkuu hatimaye.

Kupitia kwa moto ni jambo linaloogofya. Linatukumbusha uchungu na hata kifo. Katika Warumi 8:17, Paulo alisema kwamba tukitaka kushiriki urithi wa Yesu, lazima pia tushiriki mateso yake. Yesu aliteseka vipi? Tunatarajiwa kwenda msalabani pia? Jibu ni ndiyo na la. Si lazima tuangikwe kwenye msalaba halisi kwa ajili ya dhambi zetu, lakini katika Marko 8:34, Yesu alisema tunafaa kuchukua msalaba wetu na kumfuata. Aliendelea kusema kuhusu kuweka kando mwenendo wa maisha ambao ni wa choyo na ubinafsi. Biblia inasema tunafaa kufa nafsi. Niamini, kuondoa ubinafsi huhitaji moto- na mara nyingi mwingi sana. Lakini tukihiari kupitia moto huo, tutajua baadaye furaha ya kumletea Mungu utukufu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anakupenda sana na ataendelea kufanya kazi ndani yako hadi siku yake ya kurudi.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon