Kuruhusu Upendo Kushinda Vita

Kuruhusu Upendo Kushinda Vita

Maana inagawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. —WAKORINTHO 10:3–4

Bila shaka tuko vitani. Biblia inatufundisha kwamba silaha za vita vyetu si za mwili, silaha za kawaida, lakini zile zilizo na nguvu kupitia kwa Mungu hata za kuangusha ngome.

Sehemu ya kumkaribia Mungu ni kufanya kazi na Roho Mtakatifu katika kuangusha ngome za ubinafsi, kiburi, na umuhimu wa kibinafsi. Kwa kukusudia kutoa kukosa kujitazama na kumfanyia mtu mwingine kitu huku tukidhurika ni mojawapo ya vitu muhimu tunavyoweza kufanya ili kushinda uovu.

Yesu alipokuwa msalabani akiwa katika kilele cha mateso yake, alichukua muda kumfariji mwizi aliyekuwa kando yake (Luka 23:39- 43). Stefano alipokuwa akipigwa kwa mawe, aliwaombea waliokuwa wakimpiga kwa mawe, akimwambia Mungu asiwahesabie dhambi (Matendo ya Mitume 7:59-60).

Iwapo kanisa la Yesu Kristo, mwili wake hapa ulimwenguni, utapigana vita dhidi ya ubinafsi na kutembea katika upendo, ulimwengu utaanza kutambua.


Kutembea kwa upendo ni sehemu muhimu ya vita vya kiroho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon