
Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. YOHANA 12:25
Tunapoamini kuwa Mungu anatutaka kufanya kitu, mara nyingi tunaanza kwa maswali: Ni kitu gani nitalazimika kusalimisha nikifanya hivi? Nikifanya hivi itanigharimu kitu gani? Nikifanya hivi, itaniondoleaje raha?
Ukweli ni kwamba kitu chochote tunachomfanyia Mungu huhitaji uwekezaji. Sehemu moja ya kumpenda huhusisha hiari ya kusalimisha nafsi zetu kwake. Iwapo Mungu amekuwa akikwambia ufanye kitu na umekuwa ukiahirisha kwa sababu unajua kitahitaji kujitolea upande wako, ninakuhimiza kukifanya. Hakuna hisia nzuri kama kujua umemtii Bwana kikamilifu.
Usiogope kujisalimisha Mungu anapokuita au kuweka kitu moyoni mwako ambacho anataka ufanye. Mpango wake juu ya maisha yako ni mkubwa kuliko kitu chochote unchoweza kufikiria. Shukuru kwamba mpango ni mzuri sana na udhamirie kwamba utalipa gharama na kupita mtihani. Ninakuhakikishia kwamba inastahili.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwamba hakuna kujisalimisha nitakakofanya kwa ajili yako kutawahi kuwa bila faida kubwa kwa maisha yangu. Nijaze na imani na nguvu za kufanya yote ambayo umeniita kufanya. Ninachagua kutii sauti yako katika eneo la maisha yangu.