Kusamehe Mungu

Kusamehe Mungu

Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; nitanena kwa mateso ya roho yangu; nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu. —AYUBU 7:11

Kama Ayubu, watu wengi wana matatizo ya kumlaumu Mungu kwa mashaka yao. Wana hasira na Mungu! Huenda wale ambao hawajawahi kupitia hisia kama hizo wasielewe. Lakini kuna wale ambao wamejua vile inavyohisi kumchukia Mungu kwa sababu wanamlaumu kwa kukosa kuwapa kitu fulani cha maana katika maisha yao. Mambo hayakuenda vile walivyopanga. Wanaamini kwamba Mungu angebadilisha mambo iwapo angetaka, lakini kwa sababu hakufanya hivyo, wanahisi kusikitika na kumlaumu kwa hali yao.

Iwapo unashikilia fikra kama hii, lazima utambue kwamba ni vigumu kuwa na uhusiano wa karibu na mtu uliyekasirikia. Mungu ndiye anaweza kukusaidia, kwa hivyo jibu la pekee ni kuacha hasira. Maisha yakikusikitisha, mkimbilie Mungu, sio kumtoroka.

Mara nyingi huwa tunafikiri iwapo tungejua kwa nini vitu fulani huwa vinatufanyikia, tungeridhika. Ninaamini Mungu hutuambia tu kile ambacho tunahitaji tu kujua, tulicho tayari kushughulikia, na kisichotudhuru lakini kitakachotusaidia. Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kujifunza kusahau na kutojaribu kuwaza kuhusu kila kitu maishani.


Lazima wakati ufike ambapo tutaacha kuishi katika siku za nyuma na kuuliza kwa nini. Badala yake, tunaweza kujifunza kuacha Mungu ageuze makovu yetu kuwa nyota.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon