Kusamehe Wengine

Kusamehe Wengine

Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. —WAEFESO 4:32

Wakati mmoja nilisikia kuwa tafiti za kimatibabu zinaonyesha kwamba, asilimia 75 ya magonjwa ya mwili yanasababishwa na matatizo ya kihisia. Na mojawapo ya matatizo makubwa ya kihisia ambayo watu hupitia ni kuhukumika. Wao hukataa kutulia na kufurahia maisha kwa sababu, hata hivyo wanahisi hawastahili kuwa na wakati mzuri. Kwa hivyo wanaishi katika mvuto wa mara kwa mara wa majuto na kujuta. Aina hii ya mfadhaiko hufanya watu wawe wagonjwa.

Vitu viwili vinavyotufanya tufungike ndani ni kutafakari kuhusu mambo yote hasi tunayofanyiwa na wengine, na dhambi na mambo mabaya tuliyofanya. Huwa tunakuwa na muda mgumu kusahau mabaya tuliyofanyiwa na wengine na tunapata ugumu wa kusahau makosa tuliyofanya.

Katika maisha yangu nilikuwa na chaguo la kubaki na uchungu, mwingi wa chuki na kujihurumia, kuchukia watu walionidhuru au kuchagua kufuata njia ya Bwana ya msamaha. Huu ndio uteuzi ulio nao leo. Ninaomba kwamba utawasamehe wengine na kupokea msamaha wa Bwana wewe mwenyewe. Utakuwa mwenye afya na furaha zaidi ukifanya hivyo!


Njia ya Mungu ni msamaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon