Kusimama Imara

Kusimama Imara

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. WAEFESO 6:13–14

Imani huwa thabiti, lakini hofu hutoroka. Tunaruhusu hofu kututawala tukitoroka kile Mungu anataka tukikabili. Waisraeli walipokuwa wamemwogopa Farao na jeshi lake, Mungu alimwambia Musa kuwaambia “Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana” (Kutoka 14:13).

Hatutawahi kuona au kuwa na nguvu za Mungu za ukombozi tukiwa na woga wa kufanya vitu. Simama na uone kile Mungu atakufanyia. Mwamini, shukuru kwa uaminifu wake, na umpe nafasi ya kuonyesha nguvu na wema wake kwako.

Hofu ikibisha mlangoni, itume imani kujibu. Usiongee hofu zako; ongea imani. Sema kile Mungu atasema katika hali yako—sema kile Neno lake linasema, sicho kile unachohisi au kufikiria.


Sala ya Shukrani

Nisaidie, Baba, kusimama imara ninapohisis mfadhaiko au hofu. Ninakushukuru kwamba kwa sababu uko nami, sina cha kuhofu. Leo, nitaamua kusimama imara badala ya kusita nikihisi woga katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon