Na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo. WAEFESO 5:20
Katika Biblia nzima, tunaona watu wakisherehekea maendeleo na ushindi kwa njia nyingi. Mojawapo ya njia hizo ilikuwa ni kutenga muda maalum kumpa Mungu sadaka na kumshukuru. Noah alifanya hivyo. Ibrahimu alifanya hivyo. Na tunaweza kufanya hivyo pia.
Tunaweza kuongeza haraka muda wa sherehe katika maisha yetu iwapo tutatenga muda kutoa shukrani Mungu anapotufanyia vitu vya ajabu. Desturi ya kushukuru huonyesha mengi kuhusu tabia za mtu. Shukrani humtanguliza Mungu, tukijua kwamba ni chanzo cha kila baraka tunayopokea. Shukrani haihusu kuhisi kwamba tuna haki—ni fikra zinazosema, “Ninajua sistahili wema wa Mungu, lakini kwa hakika ninashukuru kwa ajili ya wema huo.”
Sala ya Shukrani
Baba, nimejawa na shukrani kwa kuwa umenibariki na vitu vingi vizuri katika maisha yangu. Leo, ninachukua muda kutafakari juu ya wema wako na kukushukuru kwa baraka zako.