
Wewe umeonyeshwa haya ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. —KUMBUKUMBU LA TORATI 4:35
Kukosa maarifa husababisha hofu, lakini hakika ya hakikisho la maarifa huondoa hofu na kuleta nguvu na ujasiri. Acha nikupe mfano:
Usiku mmoja miaka mingi iliyopita, nilikuwa nimelala kitandani na nikasikia sauti zisizo za kawaida zikitoka mahali nyumbani. Kadri nilivyosikiliza kwa muda mrefu, ndivyo nilivyozidi kuingiwa na woga. Mwishowe huku nikitetemeka kwa hofu, nilitoka kwenye chumba cha kulala, kuangalia kilikuwa kitu gani. Nilicheka nilipogundua kwamba vilikuwa vidonge vya barafu vikianguka kwenye sinia ya barafu kutoka kwa kitengeneza barafu. Kwa sababu fulani vilikuwa vikifanya kelele ambayo kawaida havikuwahi kufanya. Kwa sababu sikujua kilichokuwa kikifanya kelele hizo, nilikuwa mwoga tu bure.
Hivi ndivyo watu wanavyohisi katika maisha yao mara nyingi. Hawajui kwamba Mungu anawapenda, yuko nao, na amewapa kila kitu wanachohitaji, kwa hivyo wanaogopeshwa na vitu vingi. Wanaposikia kwamba mtu hawapendi, wanashikwa na woga. Wanaposikia ripoti mbaya katika habari za jioni wanashikwa na hofu.
Iwapo una maarifa kuhusu Mungu ni nani na wewe ni nani katika Kristo, hofu haitakuwa na nafasi yoyote katika maisha yako. Haijalishi vile hali inaonekana nje, utakuwa na amani moyoni mwako, hakika iliyo na hakikisho linalojaza kila eneo la maisha yako.
Sauti zisizo za kawaida za ulimwengu zinapojaribu kukujaza hofu, kuwa na hakika kwamba Mungu yuko nawe.