Kutiwa Nguvu Kupitia kwa Sifa

Kutiwa Nguvu Kupitia kwa Sifa

Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; ndiye Mtakatifu! Zaburi 99:3

Kuna nguvu kuu katika sifa. Tunapata nguvu zaidi na zaidi, imani yetu inaongezeka na vitu vinavyokuja kutushinda vinaharibiwa tunapomsifu Mungu. Kufurahia sifa nzuri na nyimbo za ibada ni mojawapo ya vifaa tulivyonavyo vya kutusaidia kuishi katika mazingira ya sifa.

Kila wakati tunapokuwa na nafasi—hata dakika moja au mbili tunapotembea sehemu za maegeshoni hadi madukani, au tukingoja kwenye foleni kulipia—tumia nafasi hiyo kumsifu na kumwabudu Mungu. Baada ya muda mfupi, sifa huwa kitu cha kawaida kiasi kwamba inamiminika kutoka kwetu bila kukusudia. Tunajipata tukiimba na kumshukuru Mungu kama mwitiko tunaofanya bila kufikiri ambao hutokana na ufahamu wetu wa wema, rehema na neema zake.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kufikia mahali ambapo sifa itakuwa kawaida yangu. Asante kwa kuwa ninaweza kukutazama wewe na wema wako badala ya shughuli za dunia. Ninashukuru kwa uwepo na nguvu zako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon