Kutoa Mshinikizo kwa Watu Wengine

Kutoa Mshinikizo kwa Watu Wengine

Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote. —1 TIMOTHEO 2:1

Upendo na kukubaliwa ni mahitaji aliyo nayo kila mtu. Hili linajumlisha watu walio katika maisha yetu. Tukidai kwamba lazima watu wabadilike na kuwa zaidi kama sisi au kuwiana na kile tunachopenda, tunaweka mkazo mkubwa kwenye mahusiano hayo.

Ninakumbuka miaka niliyojaribu kwa kumbadilisha mume wangu, Dave, kwa nguvu, na kila mtoto wetu kwa njia tofauti. Hiyo ilikuwa miaka ya masikitiko, kwa sababu yote niliyojaribu hayakufanya kazi. Jitihada zangu za kubadilisha watu niliowapenda hazikuwa zinasaidia mambo. Badala yake nilikuwa nikiharibu mambo kabisa.

Kama wanadamu, sisi wote tunahitaji nafasi na uhuru, wa kuwa jinsi tulivyoumbwa kuwa. Tunataka kukubaliwa jinsi tulivyo. Hatutaki watu kutupatia ujumbe kwamba lazima tubadilike ndipo tukubalike au tupendwe.

Hili halimaanishi tukubali dhambi katika watu wengine na kuivumilia tu. Inamaanisha tu kwamba njia ya kubadilika ni maombi, sio mshinikizo. Tukipenda watu, na kuwaombea, Mungu atafanya kazi. Ili mabadiliko yadumu, lazima yatoke ndani hadi nje. Ni Mungu pekee anayeweza kusababisha aina hiyo ya mabadiliko ya moyo.


Kusumbua sio kifaa cha mafanikio kwa mabadiliko. Ni maombi tu na upendo wa Mungu utakaofanya kazi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon