Kutosha zaidi ya Kutosha

Kutosha zaidi ya Kutosha

Ikiwa mioyo yetu inatuhukumu kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. —1 YOHANA 3:20

Lawama na hukumu ni matatizo makubwa kwa waaminio wengi. Furaha kubwa ya shetani ni kutufanya tuhisi vibaya kujihusu. Huwa hatwambii umbali ambao tumetoka, badala yake, hutukumbusha bila kukoma umbali ambao bado tunaenda.

Adui anaposhambulia, unaweza kumwambia, “Siko ninapohitaji kuwa, lakini shukuru Mungu siko nilipokuwa. Niko sawa, na niko njiani.”

Kama Daudi, tunaweza kujifunza kujihimiza ndani ya Bwana (1 Samweli 30:6). Hakuna mmoja wetu aliyewasili katika hali ya utimilifu na hatuwezi kujitimilisha. Usafishaji unafanywa ndani yetu kwa Roho Mtakatifu kama mchakato, kwa hivyo jifunze kufurahia mchakato huo. Biblia inafundisha tunaweza kuwa na msamaha kamili wa dhambi zetu (uhuru mkamilifu kutokana na kuhukumika) kupitia kwa damu ya Yesu Kristo. Hatuna lazima ya kuongeza hatia yetu kwa dhabihu yake. Anatosha zaidi ya kutosha.

Tayari Yesu amefanya kila kitu kinachohitaji kufanywa—kazi imeisha. Ametengeneza njia ya wewe kusamehewa. Unachofaa kufanya ni kuupokea. Msamaha mkamilifu ni uhuru mkamilifu!


Usimruhusu shetani kujaza kichwa chako na mawazo ya kutofaa kama mwenye dhambi. Anza kujiona kama mwenye haki wa Mungu ndani ya Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon