Kuunda Orodha Iliyojaa Shukrani

Kuunda Orodha Iliyojaa Shukrani

Ingieni malangoni mwake kwa kusifu; nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake! ZABURI 100:4

Ili kukusaidia kupata na kudumisha kiwango kipya cha ridhaa katika maisha yako, ninakuhimiza kuunda orodha ya vitu vyote unavyofaa kushukuru kwavyo. Ifanye iwe orodha ndefu inayojumlisha vitu vidogo, na vitu vikubwa vile vile. Inafaa kuwa ndefu kwa sababu sisi wote tuna vitu vya kushukuru kwavyo tukivitafuta. Mimi hupata vitu vipya vya kumshukuru Mungu kwavyo na nina hakika utapata pia.

Toa karatasi sasa hivi, au tumia kompyuta yako na uanze kuorodhesha vitu unavyofaa kushukuru kwavyo. Weka orodha hiyo na uongezee kila mara. Fanya iwe kawaida yako kufikiri kuhusu vitu ambavyo unashukuru kwavyo unapowaendesha watoto hadi kwenye shughuli fulani au ukiwa kwenye foleni dukani. Unaweza tu kujifunza “nguvu za asante” kwa kutumia. Biblia inasema tuwe wenye shukrani na kusema. Kutafakari kuhusu kile unafaa kushukuru kwacho kila siku na kukisema itakusaidia kwa njia ya ajabu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa upaji mwingi ulionibariki nao maishani mwangu. Nina mengi ya kushukuru kwayo kwa sababu ya wema wako mkuu. Nisaidie nisiwahi kupuuza kitu chochote kiwe kidogo au kikubwa—na kuviona kuwa vya kawaida.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon