Kuwa Jasiri

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. — WAEBRANIA 4:16

Ukiomba na mimi niombe, tunafaa kwenda kwa Mungu kama waaminio wala si kama ombaomba. Kumbuka kwamba kulingana na Waebrania 4:16, tunaweza kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri: sio kama ombaomba, lakini kwa ujasiri; sio kwa vita.

Hakikisha una kiasi. Kuwa mwenye heshima, lakini kuwa jasiri. Mkabili Mungu kwa ujasiri. Amini kwamba anafurahia maombi yako na yuko tayari kujibu maombi yoyote ambayo yanalingana na mapenzi yake.

Kama waaminio, tunafaa kujua Neno la Mungu, ambalo ni mapenzi yake. Kadri tunavyojifunza Neno la Mungu ndivyo tunavyopata ujasiri katika kuomba.

Mimi na wewe tunapozidi kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha neema, na kuomba kwa imani kulingana na Neno lake na kwa jina la Mwanawe Yesu Kristo, tunaweza kujua kwamba tumepata majibu ya maombi yetu. Sio kwa sababu sisi wenyewe ni wakamilifu au tunastahili, au kwa sababu Mungu anatudai kitu, lakini ni kwa sababu anatupenda na anataka kutupatia tunachohitaji katika maisha.


Yesu ametununulia urithi wenye utukufu kwa kutitirika kwa damu yake. Kama warithi pamoja naye, tunaweza kuomba kwa ujasiri.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon