Kuwa Yule Mungu Alikuumba Kuwa

Kuwa Yule Mungu Alikuumba Kuwa

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. MWANZO 1:27

Watu wengi wanaogopa kuwa tofauti na watu wengine. Wanakuwa na utulivu katika kufuata umati kuliko kuthubutu kufuata uongozi wa Roho wa Mungu. Tukifuata mfano wa watu wengine, huenda tukawapendeza, lakini tukitoka nje kwa imani na kufuata Roho wa Mungu, tunampendeza.

Kuna ridhaa inayokuja tunapojifunza kujitanzua kutoka kwa vitu vilivyotufunga, niseme hivyo, na kuruhusu bahari ya Roho wa Mungu kutupeleka anakohiari. Tunapokuwa kwenye udhibiti, tunang’ang’ana kuamua kitakachofanyika, lakini tukiruhusu Roho wa Mungu kuongoza, tutashuhudia vitu vingi vya kushangaza vilivyoamriwa na Mungu katika maisha.

Tunaweza kushukuru kuwa Mungu ana mpango wa kipekee wa kibinafsi kwa kila mmoja wetu! Acha tudhamirie kuwa tulivyo na tukatae kuishi maisha yetu tukiwa tunajiona duni kwa sababu tu tuko tofauti na watu wengine.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa upekee wangu. Ninashukuru kuwa sihitaji kufuata umati katika maisha—kile ninafaa kufanya ni kukufuata. Leo, nitakutazama wewe na sio wengine. Niongoze na unielekeze ninapokufuata kwa moyo wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon