Kuwekeza katika Ndoto Yako

Kuwekeza katika Ndoto Yako

Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu, bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa. MITHALI 13:4

Ndoto za mustakabali zinaweza kutimia, lakini sio kile ninachoita “uongo chanya.” Kwa maneno mengine, zinawezekana, lakini hazitafanyika kwa njia chanya tusipofanya sehemu yetu.

Watu wengi sana huchukua njia fupi ya kufanya kila kitu kwa haraka. Wao hutaka tu kinachowafanya kuhisi vizuri sasa hivi. Hawahiari kuwekeza kwa ajili ya mustakabali wao. Lakini unaweza kuwa tofauti! Iwapo unahiari kufuatilia kile Mungu ameweka ndani ya moyo wako, atabariki bidii yako. Unaweza kushukuru, ukijua kwamba ukifanya kile Mungu anataka ufanye, wakati wote atafanya kile yeye peke yake anaweza kufanya.

Huwa kuna mgodi wa dhahabu uliofichika katika kila maisha, lakini lazima tuuchimbe ili kuifikia. Hiari kuchimba zaidi na ukiuke jinsi unavyohisi au kinachokutuliza ili uone ndoto zako zikitimia.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru Baba, kwamba nikiwa na bidii nawe ukiwa upande wangu, yanayowezekana yanaweza kugeuka kuwa “uongo chanya.” Licha ya kazi nyingi inayohitajika, nitafuatilia kile ulichoweka katika moyo wangu. Asante kwa kuwa nikifanya sehemu yangu, unaahidi kufanya sehemu yako pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon