Kuzoeza Musuli wa Kiasi

Kuzoeza Musuli wa Kiasi

Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi na katika kiasi chenu subira na katika subira yenu utauwa. 2 PETRO 1:5–6 BIBLIA

Mojawapo ya makosa makubwa tunayoyafanya ni kufikiri kwamba hatuna udhibiti dhidi ya vile tunavyohisi au kile tunachofanya. Mungu ametupatia roho wa nidhamu na kiasi, na inaitwa kiasi kwa sababu Mungu hutupatia kifaa hiki kujidhibiti binafsi. Sisi wote tunacho lakini je, tunakitumia?

Kitu chochote tulicho nacho lakini tusichotumia hufifia na kukosa nguvu. Je, huwa unafanya mazoezi kila mara? Wewe hufanya hivyo kwa nini? Unafanya mazoezi ili kuimarisha mifupa yako na misuli—kulinda afya yako. Shukuru kuwa Mungu ametupatia kiasi, na tunaweza kukitumia kulinda afya yetu ya kiroho, kihisia na kimwili. Lakini tunaweza kutumia musuli huo ili ufanye kazi vizuri. Tunapofanya hivyo tunaanza kuwa na kiwango kipya cha nguvu ambacho kiasi peke yake kinaweza kuleta. Kiasi ni rafiki yako, sio adui. Kinakusaidia kuwa mtu yule ambaye unataka kuwa kweli.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa nina kiasi. Nisaidie kuishi maisha ya kiasi na kumfuata Roho wako badala ya mwili wangu. Asante kwa sababu kwa usaidizi wako, ninaweza kuwa na ushindi dhidi ya mwili na kuishi katika uhuru wa Roho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon