Lakini huko, kama mkitafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. KUMBUKUMBU LA TORATI 4:29
Tunapofikiria kuhusu vile watu wengi humpa Mungu wakati mchache, tunaweza kuelewa kwa nini Biblia inatuhimiza kwa nguvu kumtafuta. Ukweli ni kwamba tunakosa kitu kikubwa maishani iwapo hatutawahi kupata kumjua Mungu kibinafsi.
Mtume Paulo alisema kwamba kusudi alilodhamiria ni kumjua Mungu na uweza wa kufufuka kwake (tazama Wafilipi 3:10). Neno tafuta lina nguvu sana. Katika l ugha yake asilia, lina maana ya “kutamani; kufuata; kufuatilia kwa nguvu zako zote.”
Tunaweza kushukuru kuwa Mungu wetu ni Mungu wa ajabu anayestahili kutafutwa. Anastahili kupendwa! Anastahili mapenzi na ibada yako yote. Kwa hivyo usingoje hadi ujipate katika hali ya kukatisha tamaa. Dhamiria kutafuta na kumpenda Mungu kwa moyo wako wote kuanzia sasa.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Baba, kwamba ninaweza kukutafuta kwa moyo wangu wote na kuishi katika uhusiano wa karibu nawe. Kama Paulo, ninataka kulifanya kusudi langu nililodhamiria kukujua. Ninakushukuru kuwa unanipenda na unanituza kwa uwepo wako ninapokutafuta.