Kwa nini Mungu mwema huacha mambo mabaya kutokea?

Kwa nini Mungu mwema huacha mambo mabaya kutokea?

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Yakobo 1:17

 Tunapopatwa na msiba mkubwa, kumkasirikia Mungu ni jambo la kawaida. Watu huuliza mara nyingi, “Ikiwa Mungu ni mzuri, mwenye nguvu zote, na mwenye upendo kwetu, kwa nini aliacha kitu kilichosababisha maumivu?”

Hapo Shetani anataka kujenga ukuta kati ya Mungu na mtu aliyeumia . Anachukua fursa ya kusema, “Mungu si mzuri, na hawezi kuaminiwa.” Hata hivyo, tunajua kulingana na Neno la Mungu, ukweli hauko katika Shetani – yeye ni mwongo na baba wa uongo .

Soma Yakobo 1:17. Kila kitu kizuri hutoka kwa Mungu. Mungu ni mwema, na Yeye hawezi kuwa vingine. Zaidi ya hayo, Yeye habadiliki. Yeye ni imara kabisa, mwaminifu na thabiti. Yeye ni mzuri-wakati wote.

Ni dhahiri kwamba Mungu hawezi kuzuia kila msiba, na kwa kweli hatujui ni kwa nini mambo mabaya yanatokea. 1 Wakorintho 13:12 inasema, … Sasa najua kwa sehemu (bila ya kutosha) … Tunapaswa kukumbuka kwamba imani daima itatutaka tukubali maswali yasiyojibiwa na lazima tufikie mahali ambapo tunastahili kumjua Yeye ambaye anajua yote, na kuweka imani yetu kwake.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, siwezi kila mara kuelewa kwa nini mambo mabaya yanatokea, lakini najua wewe ni mwema. Wakati sielewa ni kwa nini, nitapata faraja yangu kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon